Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan pande zote kushirikiana mafuta

2b787a0034c89e645d7eddf80e33ce05.jpeg Sudan pande zote kushirikiana mafuta

Tue, 13 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SUDAN na Sudan Kusini zimekubaliana kushirikiana katika sekta ya mafuta.

Makubaliano hayo yalifikiwa wakati wa mkutano wa kati ya Waziri wa Nishati na Mafuta wa Sudan, Gadain Ali Ebaid na mwenzake wa Sudan Kusini, Puot Kang.

Wakati wa makubaliano hayo, Ebaid alisema sekta ya mafuta ni kipaumbele kwa watu wa nchi hizo mbili na kutaka kuwekwa mikakati zaidi katika ushirikiano wa nchi hizo katika sekta hiyo.

Septemba mwaka jana, Sudan na Sudan Kusini zilitia saini makubaliano ya rasimu ya kukuza ushirikiano katika sekta ya mafuta.

Aidha, nchi hizo zimekubaliana kuimarisha uhusiano kwa kuwezesha harakati za biashara, uwekezaji na ushirikiano wa kiuchumi.

Uamuzi huo ulifikiwa kati ya Waziri wa Uwekezaji wa Sudan, Dk Al-Hadi Mohamed Ibrahim na mwenzake wa Sudan Kusini, Dhieu Mathok.

Ibrahim alisema ushirikiano wa kati ya nchi hizo mbili ni miongoni mwa vipaumbele vya serikali.

Kwa upande wake, Mathok alitaka kudumishwa ushirikiano wa karibu na uratibu kati ya wizara hizo mbili na kufunguliwa tena kwa mipaka kati ya nchi hizo mbili.

Chanzo: www.habarileo.co.tz