Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan na Ethiopia kwenye mvutano kufuatia kukutwa miili 29 mtoni

Bodies Ethp Sudan yaitupia lawama Ethiopia Matukio ya kuokotwa miili katika kingo za Mto

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali nchini Sudan, imeitupia lawama Ethiopia kufuatia kukutwa kwa miili ya watu waliofariki dunia ikielea katika Mto unaotiririka kutoka nchini Ethiopia.

Malalamiko hayo yamewasilishwa katika ubalozi wa Ethiopia uliopo mjini Khartoum, mara baada ya kupatika kwa miili 29 iliyokuwa iki elea katika kingo za mto huo.

katika Tarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya nchini Sudan inaeleza kuwa miili hiyo ilitambuliwa kuwa ni ya raia wa Ethiopia huku wakishuku kuwa ni ya kikundi cha waasi cha Trigay.

Hata hivyo Balozi wa Ethiopia nchini humo aliwahi kuitwa na Wizara hiyo mara kadhaa kwa tukio hilo hilo la kukutwa kwa miili katika kingo za mto huo kati tarehe 26 Julai, Agosti 08 na 30 mwaka 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live