Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan kufikwa na yaliyotokea Libya?

Maelfu Wanatoroka Mauaji Mapya Ya Kikabila Huko Darfur Nchini Sudan Sudan kufikwa na yaliyotokea Libya?

Tue, 21 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ikiwa ni takribani miezi 7 tangu vita vianze nchini Sudan na kusababisha vifo vya maelfu ya raia na mamilioni wengine kukimbia makazi yao, wataalamu wameonya kuwa huenda taifa hilo likasambaratika kama kilichotokea nchini Libya.

Onyo lao limekuja wakati huu Jumuiya ya kimataifa ikijaribu kuongeza shinikizo kwa jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF, kusitisha mapigano.

Licha ya wito wa kusitishwa kwa mapigano kutoka kwa Jumiya ya kimataifa, pande hasimu kwenye taifa hilo zimeendelea kukabiliana katika maeneo tofauti, kila upande ukiituhumu mwengine kwa kuanzisha mashambulio.

Lakini je, suluhu inaweza kupatikana? Hamduni Marcel ni mtaalamu wa siasa za kimataifa anaangazia hili akiwa Tanzania.

‘‘Haiwezekani kupatikana suluhu kama watengenezaji wa fitina hii hawajaamua imemalizike, hilo ni jambo ambalo linastahili kuangaliwa sana.’’ alisema Hamduni Marcel ni mtaalamu wa siasa za kimataifa anaangazia hili akiwa Tanzania.

Maelfu ya raia wa Sudan wametoroka mapigano yao wengi wakipewa hifadhi katika nchi jirani ikiwemo Chad na Sudan Kusini.

Takwimu za mashirika ya kiraia zinaonyesha kuwa mamia ya watu wameuwa katika mapigano hayo yanayoendelea kati ya wapiganaji wa RSF na jeshi la Sudan. Wataalam wanaonya kuwa huenda kilichotokea nchini Libya kikatokea nchini Sudan Wataalam wanaonya kuwa huenda kilichotokea nchini Libya kikatokea nchini Sudan © Zohra Bensembra / Reuters

Mazungumzo ya kujaribu kumaliza mzozo unaoendelea ambayo yanaoongozwa na Marekani na Saudi Arabia yamekuwa yakiendelea jijini Jeddah yakionekana kutozaa matunda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live