Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan inashtumu Umoja wa Falme za Kiarabu kuwasaidia waasi wa RSF

Sudan Inashtumu Umoja Wa Falme Za Kiarabu Kuwasaidia Waasi Wa RSF Sudan inashtumu Umoja wa Falme za Kiarabu kuwasaidia waasi wa RSF

Wed, 19 Jun 2024 Chanzo: Voa

“Umoja wa Falme za Kiarabu unapaswa kujiepusha na kuingilia kati masuala ya Sudan,” Balozi wa Sudan, Al-Harith Idriss Al-Harith Mohamed ameliamba Baraza hilo.

“Hili ni sharti la kwanza ambalo litaruhusu uthabiti nchini Sudan. Umoja wa Falme za Kiarabu unatakiwa kusitisha msaada wake kwa RSF,” aliongeza.

Mohamed ameshtumu Umoja wa Falme za Kiarabu kusaidia wapiganaji wa RSF kupitia wanamgambo nchini Chad, Kusini mwa Libya na Afrika ya Kati, akiongeza kuwa Sudan iliwasilisha kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hati kadhaa za kusafiria za Umoja wa Falme za Kiarabu zilizogunduliwa kwenye uwanja wa mapigano mjini Khartoum.

Alisema pia bila kutoa ushahidi kwamba wapiganaji wa RSF waliojeruhiwa wanasafirishwa kwa ndege hadi Dubai ili kupewa matibabu.

Balozi wa Emirati Mohamed Abushabab, ambaye alikuwa amekaa kando ya mwenzake wa Sudan kwenye meza ya wajumbe 15 wa Baraza la Usalama, wakati wa mkutano kuhusu hali nchini Sudan, ameyataja madai hayo kuwa “ya kipuuzi.”

Chanzo: Voa