Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan Yatangaza Hali ya Hatari

SUDAN 1 Sudan Yatangaza Hali ya Hatari

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Ripoti za jeshi kuchukua mamlaka nchini Sudan ni “pigo kubwa ” kwa kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia, limesema Shirika la haki za binadamu, Human Rights Watch.

Sudan kwa sasa inaongozwa na baraza huru la pamoja la Jeshi na raia, kundi la jeshi lilipangiwa kukabidhi uongozi kwa baraza huru la Kiraia mwezi ujao. Human Rights Watch linasema “Jamii ya kimataifa inapaswa kushinikiza kurejea kwa kipindi cha mpito cha raia.”

Shirika hilo limevitaka vikosi vya usalama nchini humo kulinda haki za raia na kuacha kutumia mabavu, mkuu wa jeshi, Luteni Jenerali, Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, anatarajiwa kuhutubia taifa muda mfupi ujao.

Jenerali anayeongoza Sudan atangaza hali ya hatari wakati wa mapinduzi. Mkuu wa Baraza Kuu la Sudan Jenerali, Abdel Fattah Abdelrahman Burhan amevunja baraza hilo na baraza la mawaziri na kutangaza hali ya hatari nchini kote, alitoa tangazo hilo kwenye hotuba ya moja kwa moja kupitia runinga.

Wanachama wote wa Baraza Kuu wanaosimamia mabadiliko ya utawala wa kidemokrasia wameondolewa kutoka kwa nyadhifa zao, alisema, pia alivunja serikali zote za majimbo na kuwaondoa magavana kutoka kwenye  nafasi zao.

Alisema kuwa serikali ya muda itatangazwa kabla ya mwisho wa Novemba, na kutangaza kwamba uchaguzi mkuu wa kufungua njia ya serikali ya kiraia utafanyika mnamo Julai 2023.

Safari za ndege za kwenda na kutoka katika mji mkuu Khartoum zimesitishwa, huku kukiwa na taarifa za mapinduzi.

Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum umeripotiwa kufungwa na mawasiliano katika uwanja huo yamezuiwa, huku wanajeshi wakiripotiwa kuuzingira, hakuna tangazo rasmi la serikali kuhusu hali hiyo ya uwanja wa ndege.

Shirika la habari la Reuters limepata picha za waadamanaji waliokusanyika kwenye mitaa ya mji mkuu wa Sudan Khartoum Jumatatu asubuhi hii kukiwa na ripoti kwamba jeshi limechukua mamlaka ya nchi.

Picha hizo zilionyesha umati wenye hasira ukichoma magurudumu ya magari kwenye mitaa ya mji huo, wanajeshi wamepelekwa katika maeneo yote ya mji huo na wanadhibiti matembezi ya raia, limeripoti shirika la Reuters.

Chanzo: globalpublishers.co.tz