Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Wafungwa watoroka magerezani

160223 Malakal Sudan Tease Uisbiv 1140x640 Sudan: Wafungwa watoroka magerezani

Wed, 26 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maafisa wa zamani wanaozuiliwa kutoka kwa utawala wa Rais aliyepinduliwa Omar al-Bashir wameripotiwa kukimbia kutoka katika gereza la Kober huko Khartoum, ambalo limekuwa kitovu cha vita vya kuwania madaraka nchini Sudan.

Haijulikani kama Bashir - ambaye alifungwa kwa ufisadi katika kipindi chake cha miaka 30 - ni miongoni mwa waliotoroka.

Hata hivyo, Al Jazeera siku ya Jumanne iliwataja wanafamilia wakisema bado anapokea matibabu katika hospitali ya kijeshi katika mji mkuu wa Sudan.

Na afisa kutoka chama tawala cha zamani cha National Congress Party (NCP) ambaye alikimbia kutoka gerezani aliliambia gazeti la Al-Sudani kwamba

"watajisalimisha kwa mamlaka ya mahakama hali itakaporuhusu". "Tulifanya uamuzi wa kujilinda kutokana na ukosefu wa usalama, maji, chakula na matibabu, pamoja na vifo vya wafungwa wengi huko Kober [gerezani]," Ahmed Haroun alisema.

Haroun anasakwa kwa tuhuma za uhalifu wa kivita, jambo ambalo awali amelikanusha.

Zinahusiana na madai ya uchochezi wa ghasia dhidi ya raia huko Darfur. Alikamatwa mwaka 2019 kufuatia mapinduzi dhidi ya Bashir.

Magereza yameripotiwa kulengwa huku mapigano kati ya makundi hasimu ya kijeshi yakiendelea kwa wiki ya pili.

Katika mji mkuu wa Darfur Kusini wa Nyala, wafungwa wasiopungua 750 waliripotiwa kutoroka kufuatia maandamano na ghasia za wafungwa, huku mamia ya wengine wakitoroka kutoka magereza mengine ya Khartoum na Omdurman.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live