Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Uporaji wazuka mjini Khartoum, wamiliki wa nyumba wakitoroka

Sudan: Uporaji Wazuka Mjini Khartoum, Wamiliki Wa Nyumba Wakitoroka Sudan: Uporaji wazuka mjini Khartoum, wamiliki wa nyumba wakitoroka

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Kuanzia viatu vya visigino virefu hadi seti za runinga, nguo za wabunifu hadi maharagwe ya fava, bidhaa zilizoporwa kutoka kwa nyumba na biashara katika sehemu tajiri zaidi za mji mkuu uliokumbwa na vita nchini Sudan sasa zinaonekana katika baadhi ya vitongoji maskini zaidi.

Kwa kubeba basi na ndege, takribani watu milioni mbili walikimbia Khartoum, na miji inayopakana ya Omdurman na Bahri, baada ya mzozo kuzuka mwezi Aprili kati ya jeshi na Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF).

Magenge mengi ya wahalifu na baadhi ya watu ambao walihitaji tu pesa, walivamia nyumba zao, maduka na viwanda, wakipakia kila kitu kwenye masanduku na vikapu kabla ya kurudi nyuma - au, wakati fulani, wakipanda punda zao kwenda kwenye vitongoji vyao, kingo za mji mkuu.

Uporaji huo uliendelea kwa miezi kadhaa na unaendelea hadi leo, kwani sheria na utulivu umevunjika, hakuna kituo chochote cha polisi kinachofanya kazi katika mji mkuu unaokumbwa na milipuko ya kila siku ya mabomu, makombora na risasi kati ya vikosi vinavyopigana.

Utajiri uliopatikana kwa njia haramu unaoneshwa katika sehemu za Ombada na al-Thawra - vitongoji masikini ambavyo watu wenye uwezo wa juu huko Khartoum walikuwa wakisitasita kuingia, kwa sehemu kutokana na kuogopa magenge yenye silaha yanayofanya kazi huko.

Lakini wakazi wengi wa Ombada na al-Thawra ni watu waaminifu ambao wanatoka katika jamii zilizonyimwa zaidi za Sudan. Kwa kweli hawakuwa katika nafasi ya kupanda mabasi au ndege kwenda nchi nyingine, na walibaki nyuma.

Pia wamekuwa majeruhi wa vita, watu 25 waliuawa baada ya makombora kuanguka katika wilaya ya Ombada, mwezi uliopita.

Chanzo: Bbc