Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Tunataka majadiliano zaidi mwaliko wa Marekani

Sudan: Tunataka Majadiliano Zaidi Mwaliko Wa Marekani.png Sudan: Tunataka majadiliano zaidi mwaliko wa Marekani

Wed, 31 Jul 2024 Chanzo: Voa

Wizara ya mambo ya nje ya Sudan ambayo inalitii jeshi la serikali linalopigana na wanamgambo wa RSF Jumanne ilisema kwamba “inataka majadiliano zaidi” kabla ya kukabili mwaliko wa Marekani juu ya mazungumzo ya kusitisha mapigano.

“Mazungumzo yoyote kabla kikosi cha Rapid Support Forces (RSF) kinachoongozwa na jenerali Mohamed Hamdan Dagalo kuondoa kabisa wapiganaji wake na “kuacha” kuendelea kudhibiti maeneo, hayakubaliki”, wizara hiyo ilisema katika taarifa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken wiki iliyopita alialika jeshi la Sudan na RSF kwa ajili ya mazungumzo mjini Geneva, Uswizi, yaliyopangwa kuanza Agosti 14.

Siku hiyo hiyo, Dagalo alikubali mwaliko huo na kutangaza kwamba RSF ina nia ya kushiriki mazungumzo hayo.

Jeshi linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, halikutoa msimamo kuhusu mwaliko huo.

Vita nchini Sudan vimepamba moto tangu mwezi Aprili 2023 kati ya jeshi na kikosi cha RSF na kusababisha vifo vya maelfu ya watu na kuchochea mzozo mkubwa wa kibinadamu.

Mazungumzo hayo, yanayosimamiwa pia na Saudi Arabia, yanapaswa kujumuisha Umoja wa Afrika, Misri, Umoja wa falme za Kiarabu na waangalizi wa Umoja wa Mataifa, Blinken alisema.

Yanalenga “kufikia sitisho la ghasia nchini kote na kuruhusu usambazaji wa misaada ya kibinadamu”, Blinken alisema.

Chanzo: Voa