Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan, Sudan Kusini wafungua mpaka

0359711f2d56c5a48f879d8fe0cd3fe2 Sudan, Sudan Kusini wafungua mpaka

Tue, 3 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KWA mara ya kwanza katika kipindi cha miaka tisa Sudan na Sudan kusini wamefungua mpaka wao.

Kufunguka kwa mpaka huo kuliwezesha ujumbe wa viongozi wa ulinzi na usalama kutoka Sudan Kusini kufika Khartoum.

Msemaji wa wizara ya ulinzi, Kanali Paul Gabiel alisema katika taarifa yake kwenye mtandao wa kijamii kuwa mpaka katika majimbo ya Upper Nile-White Nile umefunguliwa wakati wa hafla hiyo.

Waziri wa Ulinzi na Masuala ya Veterani, Angelina Teny na mwenzake wa Sudan, Yassin Ibrahim waliongoza ujumbe wa viongozi kutoka Sudan Kusini na Sudan kushuhudia kufunguliwa rasmi kwa mpaka kati ya nchi hizo.

Mpaka kati ya Sudan na Sudan Kusini ulifungwa mwaka 2012 baada ya mzozo wa Heglig ambao ulishuhudia vikosi vya jeshi vya Sudan Kusini, SPLA-IO, vikiumana Heglig, mji wa mpakani uliogombaniwa kwa karibu wiki mbili Aprili mwaka huo.

Septemba mwaka huo, nchi hizo mbili zilisaini mkataba wa makubaliano mjini Addis Ababa, Ethiopia, na kukubaliana kufunguliwa kwa mpaka wa nchi hizo mbili lakini mkataba huo haukufanyiwa kazi.

Mapema mwezi huu, Rais wa Baraza la Wakuu wa Mpito wa Sudan, Abdel Fattah al Burhan alisema wakati wa kusainiwa kwa makubaliano ya amani ya Sudan huko Juba kwamba wananchi wa Sudan Kusini hawatahitaji viza tena kutembelea Sudan.

Chanzo: habarileo.co.tz