Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Serikali ya Uingereza kuanza kuwahamisha raia wake

Zaidi Ya Raia 1,000 Wa EU Wamesafirishwa Kutoka Sudan Sudan: Serikali ya Uingereza kuanza kuwahamisha raia wake

Tue, 25 Apr 2023 Chanzo: Voa

Uingereza itaanza kuwahamisha Waingereza kutoka Sudan, serikali imetangaza. Familia zilizo na watoto, wazee na watu walio na hali ya kiafya zitapewa kipaumbele.

Vikosi vya kijeshi vya Uingereza vitatekeleza "operesheni hiyo tata," alisema Waziri Mkuu Rishi Sunak.

Makundi hasimu ya kijeshi yalikubali kusitishwa kwa mapigano kwa saa 72 kuanzia Jumatatu usiku nchini humo, ambapo takriban watu 400 wameuawa katika mapigano tangu tarehe 15 Aprili.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza James Cleverly alisema maafisa wameanza kuwasiliana na raia wa Uingereza. Mawaziri wamezidi kushinikizwa kusaidia takriban raia 2,000 kukimbia mapigano makali.

Bw Sunak alielezea uhamishaji huo kama "mkubwa" na alitoa pongezi kwa wanajeshi ambao wanatekeleza operesheni hiyo kuanzia Jumanne.

Takriban raia 4,000 wa Uingereza wanafikiriwa kuwa nchini Sudan na 2,000 kati yao tayari wameomba msaada, waziri wa mambo ya nje Andrew Mitchell alisema Jumatatu.

Siku ya Jumapili, Uingereza iliwasafirisha kwa ndege wanadiplomasia na familia zao kutoka Sudan katika operesheni ya kijeshi.

Chanzo: Voa