Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: RSF lawamani kwa kuzuia misaada kufika Darfur

RSF Yasema Inasonga Mbele Kuteka Sudan Nzima Sudan: RSF lawamani kwa kuzuia misaada kufika Darfur

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mashirika ya misaada pamoja na nchi ya Marekani, yamewakashifu wapiganaji watiifu kwa jeshi la Sudan, ambao wamekuwa wakizuia kuingizwa kwa misaada kwenye mkoa wa Darfur Magharibi.

Eneo hilo la mpaka na nchi ya Chad, limekuwa kitovu cha mapigano tangu vita vianze miezi 10 iliyopita, kati ya jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF.

Wapiganaji wa RSF ambao wengi wanatoka kundi la waasi wa Janjaweed, wamekuwa akiendesha kampeni ya mashambulio kwenye jimbo la Darfur miongo miwili iliyopita, ambapo linashikilia maeneo manne kati ya matano ya jimbo hilo.

Aidha kwa majuma kadhaa sasa, jeshi la Serikali limekuwa likitekeleza operesheni kujaribu kuwafurusha wapiganaji wa RSF kwenye jimbo hilo, operesheni ambazo mashirika ya misaada yanasema zimechangia kuzuia kufikisha misaada katika maeneo yanayodhibitishwa na RSF.

Kwa mujibu wa UN, zaidi ya watu laki 6 wamekimbilia kwenye mpaka wa Chad huku maelfu wakisalia Darfur na wanahitaji msaada.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live