Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: OIC imeitambua RFS kama "kikosi cha waasi"

Vikosi Vya RSF Vyadai Kuliteka Jiji La Nyala Sudan Sudan: OIC imeitambua RFS kama "kikosi cha waasi"

Mon, 2 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imetangaza kwamba Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imepitisha - kwa mara ya kwanza - uamuzi unaovitambua Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kama "kikosi cha waasi". Uamuzi huo rasmi uliotolewa na Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Nje wa jumuiya hiyo katika kikao chake cha hamsini, ambacho ilifanyika Yaoundé, Cameroon, Agosti 29 na 30.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema, uamuzi huo umethibitisha mshikamano kamili wa taasisi hiyo na Sudan katika kukabiliana na vita vinavyoendelea nchini humo tangu Aprili 2023, na kusisitiza umuhimu wa kudumisha usalama, utulivu na uadilifu nchini Sudan.

Uamuzi huo pia umeeleza kuwa Jukwaa la Jeddah linatambuliwa kuwa msingi wa mchakato wowote wa mazungumzo ya amani ya Sudan, na kutaka utekelezaji wa vipengee vyake vyote.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan, Hussein Awad Ali, amekaribisha uamuzi wa jumuiya hiyo, akiutaja kuwa ni ushindi wa kidiplomasia wa Sudan na hatua muhimu inayolitambua kundi la RSF kuwa ni "shirika la kigaidi."

Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan pia ameahidi kuendeleza juhudi katika majukwaa yote ya kimataifa na kikanda ili kufichua uhalifu wa kivita na ukiukaji wa hakki za binadamu unaofanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live