Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Msafara wa Msalaba Mwekundu washambuliwa na jeshi

Sudan Red Cross Sudan: Msafara wa Msalaba Mwekundu washambuliwa na jeshi

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza kuwa wawakilishi kadhaa wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) wamejeruhiwa baada ya msafara wao kushambuliwa na jeshi hilo wakati wakiwa katika juhudi za kuhamisha raia wa mji mkuu Khartoum. RSF iimesema, Jeshi la Sudan limeua maafisa wawili na kujeruhi wengine wawili kwenye shambulio hilo la jana.

Msemaji wa jeshi la Sudan, SAF ametangaza habari hiyo wakati akielezea masikitiko yao kuhusu ya tukio hilo na kudai kuwa, hambulio hilo limetokea baada ya msafara wa ICRC "kuiuka makubaliano na jeshi la Sudan kwa kukaribia maeneo ya jeshi hilo wakiandamana na gari lenye silaha la waasi."

Wakati huo huo, Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) jana Jumapili kililishutumu Jeshi la Sudan (SAF) kwa kushambulia msafara wa shirika hilo la Msalaba Mwekundu (ICRC), shambulio ambalo kwa mujitu wa taarifa ya RSF, limeua watu wawili na kumjeruhi mwingine mmoja.

Sudan imekuwa ikishuhudia mapigano makali ya uchu wa madaraka kati ya majenerali wa kijeshi wanaoongoza Jeshi la Sudan (SAF) na Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) mjini Khartoum na maeneo mengine ya nchi hiyo tangu Aprili 15 mwaka huu. Wanawawake na watoto ndio wahanga wakuu wa vita vya uchu wa madaraka baina ya namejerali wa kijeshi nchini Sudan

Zaidi ya watu 12,000 wameshauawa hadi sasa katika mapigano hayo, huku wengine milioni 6.6 wakiwa wamekimbia makazi yao ndani na nje ya Sudan. Hayo ni kwa mujibu wa takwimu za Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu.

Huku hayo yakiripotiwa, Sudan imewaamuru wanadiplomasia 15 wa Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) kuondoka nchini humo huku baadhi ya maafisa wa Sudan wakidai kwamba nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi inawaunga mkono wapiganaji waasi wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).

Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan jana Jumapili ilimwita Balozi Mdogo wa Imarati, Badria Alshihi na kumfahamisha kuhusu uamuzi wa kufukuzwa wanadiplomasia hao 15.

Hakuna sababu rasmi iliyotolewa ya kufukuzwa wanadiplomasia hao wa Imarati nchini Sudan, lakini hatua hiyo imekuja huku kukiongezeka mvutano kati ya Sudan na Muungano wa Falme za Kiarabu kuhusu tetesi kuwa Abu Dhabi inawaunga mkono wapiganaji hao wa RSF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live