Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Mazungumzo ya kusitisha vita kurejelewa baada ya Ramadhani

RSF Yapinga Mpango Wa Msaada Uliyofikiwa Kati Ya Jeshi La Sudan Na UN Sudan: Mazungumzo ya kusitisha vita kurejelewa baada ya Ramadhani

Wed, 27 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mjumbe maalum wa Marekani nchini Sudan Tom Perriello, amesema kuna matumaini na wawakilishi wa pande mbili zinazopigana, watarejelea mazungumzo baada ya kumalizika kwa kipindi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Perriello, amethibitisha kuwa mazungumzo hayo yatarejelewa tena Aprili tarehe 18, chini ya usimamizi wa Marekani na Saudi Arabia.

Aidha, amesema hakuna mshindi kati ya jeshi na wanamgambo wa RSF na kusisitiza umuhimu wa kufanyika kwa mazungumzo hayo ili kupata suluhu ya kudumu.

Kumekuwa na jitihada za mazungumzo yaliyoandaliwa katika mji wa Pwani wa Jedda nchini Saudi Arabia, lakini hayakuza matunda.

Mjumbe huyo wa Marekani ameonya pia nchi za kigeni zinachangia pia kuendelea kwa vita hivyo, wakati huu kukiwa na ripoti kuwa, wanamgambo wa RSF wanaungwa mkono na wapiganaji wa Wagner kutoka Urusi, huku jeshi la Sudan likiungwa mkono na Misri pamoja na Uturuki.

Ripoti zaidi zinasema, Iran nayo inaliunga mkono jeshi la Sudan.

Mapigano kati ya jeshi na RSF yalianza mwezi Aprili mwaka uliopita na mpaka sasa yamesababisha maafa ya maelfu ya watu huku mamilioni wakiyakimbia makaazi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live