Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Matumaini ya amani yazidi kufifia

Ubalozi Wa Ethiopia Nchini Sudan Waharibiwa Kwa Shambulio Sudan: Matumaini ya amani yanazidi kufifia

Sat, 14 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umeshaingia mwezi wa sita tangu vita baina ya majenerali wa kijeshi vianze huko Sudan. Vita hivyo vya vya kikatili vinaendelea kusababisha mateso yasiyokadirika, vinahatarisha maisha, kuwafukuza mamilioni ya makazi yao, na kusababisha vifo hata katika maeneo yaliyoko mbali na mstari wa mbele wa mapigano.

Mkazi mmoja wa Omdourman anayejulikana kwa jina la Rashid Mohamed Ahmed akisema: "Vita vinaendelea bila huruma. Tunaamka kila siku tukitumai kuwa suluhu au makubaliano au usitishaji mapigano utafikiwa. Kwa bahati mbaya, matumaini haya yanafifia siku baada ya siku."

Zaidi ya watu 9,000 wameshauwa, milioni 5.6 wamekimbia makazi yao na magonjwa kama ya kipindupindu yameeneo, viwanda vinaharibiwa na miundombinu yote imesambaratishwa kutokana na vita baina ya majenerali ABdel Fattah al-Burhan na Mohamed Hamdane Daglo. Miji ya Omdourman na Khartoum ndiyo iliyoathiriwa zaidi na vita hivyo.

Matumaini ya Sudan ya kumalizika vita na kurejea amani huo Sudan yanazidi kufifia huku wananchi wakizidi kuishi kwa woga.

Ni miezi sita sasa na vita baina ya majenerali wa kijeshi Sudan havina dalili ya kwisha

Mmoja wa wananchi hao, mkazi wa Omdourman aliyejitambulia kwa jina la Mona Mohamed Taher amesema: "Miezi sita iliyopita imekuwa kipindi kichungu sana kwetu. Tunaishi na hofu mchana na usiku. Tunaogopa kuangamizwa na mabomu na risasi."

Sudan imelemewa na mfumo dhaifu wa afya; vyumba vya matibabu ya dharura vina msongamano na hospitali nyingi zimefungwa kabisa.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Shirika la Kimataifa wa Madaktari Wasio na Mipaka, mzozo wa Sudan unaonyesha kushindwa jamii ya kimataifa kutatua janga kubwa linalosababishwa na pande mbili zinazopigana.

Mounira El Ser, mfanyakazi wa kujitolea katika shule ya al-Wahda anasema: "Baadhi ya mashirika ya misaada yanasaidia, lakini bado tunahitaji msaada wa afya, mablanketi na mashuka na pia kuna uhaba mkubwa wa maji na dawa. Kwa ujumla, kuna uhaba mkubwa wa huduma za afya."

Mashirika yasiyo ya kiserikali yanatoa mwito wa kuongezwa mno juhudi za kutoa misaada ya kibinadamu kwa sababu hakuna matumaini ya kumalizika vita. Mwito wa kuongezwa jitihada za kuruhusiwa wananchi wa Sudan kupata misaada ya matibabu bila vikwazo nao umeongezeka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live