Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Mataifa ya miliki za kiarabu yatuhumiwa kwa kuwahami RSF

'Tutapigana Hadi Mwanajeshi Wa Mwisho'   Kiongozi Wa RSF Wa Sudan Sudan: Sudan: Mataifa ya miliki za kiarabu yatuhumiwa kwa kuwahami RSF

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamanda wa ngazi ya juu wa nchini Sudan, ametuhumu mataifa ya miliki za kiarabu kwa kuwapa silaha wapiganaji wa RSF, ambao wamekuwa wakikabiliana na wanajeshi wa serikali kwa kipindi cha miezi 7 sasa.

Kanali Yassir al Atta, amesema wana taarifa za kijasusi kwamba mataifa hayo ya miliki za kiarabu yamekuwa yakifadhili wanapigani wa RSF ambao wamekuwa wakipigana na wanajeshi wa serikali, wakilenga kuchukuwa serikali, hili likisabisha zaidi ya watu millioni 6 kukiambia makwao wengine ma elfu wakipoteza maisha.

Atta amedai kwamba misaada hiyo imekuwa ikipitishiwa katika mataifa ya Uganda, Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Kauli yake inajiri wakati huu wapiganaji wa RSF wakiwa wamefaulu kuteka majimbo manne eneo la Durfur na sehemu ya jiji la Khartoum.

Madai haya hata hivyo yamekanusha vikali na mataifa hayo na kusema yamekuwa mstari wa mbele kupendekeza kumalizika kwa vita nchini Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live