Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan Kusini yataka kuondolewa vikwazo

Sudan Jeshiiii Malalamikp Sudan Kusini yataka kuondolewa vikwazo

Mon, 20 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sudan Kusini imeliomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea vikwazo vya silaha, kutokana na kuwa majeshi yake hayana silaha kiasi kwamba imelazimika kupeleka kikosi cha kwanza cha wanajeshi 750 katika mji wa Malakal wa jimbo la Upper Nile bila ya silaha zozote.

Michael Makuei Lueth, Waziri wa Habari na Mawasiliano, Teknolojia na Huduma za Posta wa Sudan Kusini amesema, awamu ya kwanza ya vikosi vya serikali ya umoja wa kjitaifa vilitumwa hhuko Malakal bila ya silaha kutokana na vikwazo ambavyo vimefanya iwe vigumu kwao kupata silaha.

Makuei amesema hayo mbele ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa: "Tunawapeleka bila silaha kwa sababu hatuna silaha, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeamua kupasisha azimio la kuiwekea vikwazo vya silaha Sudan Kusini, hivyo hatuwezi kupata silaha kwa ajili ya vikosi vyetu." Mahasimu wawili wa zamani wa Sudan Kusini wanaoshirikiana hivi sasa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa

Ameongeza kuwa, ni jumuiya hiyo ya kimataifa ndiyo iliyotusisitizia tupeleke askari wetu huko Upper Nile lakini tumekuwa tukisema mara kwa mara kuwa hatuwezi kupeleka vikosi vyetu bila ya silaha."

Vile vile amesema kuwa, vikosi vilivyopewa mafunzo huko Upper Nile vitapelekwa Juba ili kuunganishwa na vikosi vingine kutoka Bahr el-Ghazal. Ametoa wito kwa jamii ya kimataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo vya silaha ili kuwawezesha kuvizatiti kwa silaha vikosi vya ulinzi vya serikali ya umoja wa kitaifa.

Kundi la kwanza la wanajeshi 53,000 wa Sudan Kusini lilimaliza masomo mwezi Agosti mwaka jana. Kwa jumla wanajeshi 83,000 wanatakiwa kuhitimu mafunzo na kutumwa maeneo mbalimbali ya Sudan Kusini chini ya makubaliano ya amani yaliyoimarishwa mwaka 2018 na ambayo yalitiwa saini mwezi Disemba 2013 ili kumaliza miaka mingi ya mapigano huko Sudan Kusini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live