Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan Kusini yaondoa jeshi lake DRC

Sudan Kusini Drc Sudan Kusini yaondoa jeshi lake DRC

Mon, 11 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikai ya Sudan Kusini imetangaza kuanza zoezii la kuondoa vikosi vyake vya kulinda amani mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) hatua ambayo imefuaia ile ya Uganda ya kuanza kuondoa wanajeshi wake 1000 waliokuwa wanahudumu chini ya mwavuli wa Jumuiya ya Afrika Mashariki huko mashariki mwa DRC.

Lul Ruai Koang, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Sudan Kusini, alisema hayo jana mjini Juba na kuongeza kuwa, wanajeshi wa nchi yake waliotumwa mashariki mwa Congo mwezi Disemba 2022 kama sehemu ya Kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki.EAC wameanza kuondolewa kutoka eneo la Kivu Kaskazini nchini DRC.

Juzi Jumamosi pia, jeshi la Uganda lilianza kuondoa wanajeshi wake 1,000 waliotumwa chini ya mwavuli wa kikosi cha kulinda amani cha Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Kuondolewa askari hao wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) na wale wa Sudan Kusini kunafuatia uamuzi wa Kinshasa wa kutokiongezea muda kikosi cha kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EACRF) zaidi ya Desemba 8. Wanajeshi wa Sudan Kusini wakiwa kwenye ndege

Taarifa ya UPDF ilisema kuwa, zoezi la kuondoka wanajeshi hao linafanyika hatua kwa hatua, taratibu, na kwa muda maalumu. Zoezi hilo linatarajiwa kukamilika Januari 7, 2024.

Akitangaza taarifa hiyo Kapteni Ahmad Hassan Kato, wa UPDF ameongeza kuwa: "UPDF itahakikisha inaharakisha uondoaji wa vikosi vyake na vifaa ndani ya muda ulioainishwa katika mkutano wa dharura wa jumuiya ya EAC uliofanyika Desemba 6."

Mikutano ya dharura ya iliyofanyika mjini Arusha, Tanzania, ilikubaliana na uamuzi wa DRC na kupendekeza kwa mawaziri wa ulinzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC kwamba kazi za kikosi cha EACRF cha jumuiya hiyo ya kulinda amani huko mashariki mwa DRC kimalize rasmi shughuli zake kuanzia tarehe 8 Desemba.

Uganda, Burundi, Kenya na Sudan Kusini zilituma wanajeshi wao DRC kufuatia uamuzi uliopitishwa na viongozi wa EAC katika Kongamano la tatu la Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Amani na Usalama mashariki mwa DRC lililofanyika katika mji mkuu wa Kenya wa Nairobi mwezi Juni mwaka jana 2022. Wanajeshi wa Uganda mashariki mwa DRC

Katika sehemu nyingine ya matamshi yake, Kapteni Kato amesema: "Kikosi cha Uganda kinataka makundi yote yenye silaha huko mashariki mwa DRC kuruhusu kuondoka wanajeshi wa UPDF na kuheshimu usitishaji vita kamili."

Taarifa hiyo imeongeza kuwa: Wanajeshi wengine wa UPDF waliotumwa na serikali ya na Uganda huko mashariki mwa DRC katika operesheni ya pamoja ya kijeshi na wenzao wa Kongo wataendelea na msako dhidi ya waasi wa Allied Democratic Forces (ADF).

Kuondolewa kwa wanajeshi wa Sudan Kusini kulikuja baada ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutangaza Novemba 25 kwamba DRC haitarejesha mamlaka ya kikosi cha kanda zaidi ya Desemba 8.

Tangu Novemba 2022, kikosi hiki cha kikanda, kinachojumuisha waasi wa Kenya, Uganda, Burundi na Sudan Kusini, kimewekwa katika eneo la mashariki mwa DRC ili kukabiliana na migogoro kati ya jeshi la DRC na waasi wa Movement wa Machi 23.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live