Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan Kusini inaweza ikaathirika ikiwa vita vya Sudan vitaendelea – UN

Sudan Kusini Inaweza Ikaathirika Ikiwa Vita Vya Sudan Sudan Kusini inaweza ikaathirika ikiwa vita vya Sudan vitaendelea – UN

Thu, 25 May 2023 Chanzo: Bbc

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (Unmiss) umeonya kuwa nchi hiyo inaweza ikaathirika iwapo vita katika taifa jirani la Sudan vitaendelea.

Nicholas Haysom, mkuu wa Unmiss, aliwaambia waandishi wa habari katika mji mkuu, Juba, kwamba Sudan Kusini "itaathirika kutokana na kile kinachotokea Sudan" akibainisha kuwa athari mbaya za vita zitashuhudiwa nje ya nchi hiyo.

Alisema kukatizwa kwa bomba la mafuta la Sudan Kusini hadi Sudan - ambapo nchi hiyo isiyo na bandari inasafirisha mafuta yake yote ghafi - kutakuwa na athari za moja kwa moja.

Alisema Sudan Kusini na raia wake katika "kujikimu" wataathirika "kwa sababu 90% ya huduma na mishahara yote yanatokana na pesa za mafuta".

"Kwa hiyo katika suala hilo, bila shaka tungetaka kusema- tena kwa sauti, kwa nguvu, mara kwa mara - kwamba vita lazima vifike mwisho," Bw Haysom aliongeza.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na Kikosi cha Rapid Support Forces paramilitary (RFS), sasa yameingia katika wiki yake ya sita, na yamesababisha karibu watu milioni moja kutoroka makwao, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Idadi ya wakimbizi wa Sudan Kusini ambao wametoroka vita na kurejea nyumbani imezidi 70,000, kulingana na Unmiss.

Chanzo: Bbc