Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan Kusini imepokea msaada wa chanjo 59,520 za COVID-19

Covid 19 Vaccine Mixing Shutterstock 1891563244 Sudan Kusini imepokea msaada wa chanjo 59,520 za COVID-19

Wed, 1 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Sudan Kusini imehimiza wananchi kujitokea kupata chanjo ya COVID-19 baada ya kupokea shehena nyingine ya chanjo dozi 59,520 aina ya AstraZeneca kutoka kwenye mpango wa ugawaji chanjo Covax.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya nchini humo, Elizabeth Achuei imesema dozi hizlo zimetolewa kwa msaada kutoka serikali ya Ufaransa.

“Kwa niaba ya serikali, napenda kushukuru msaada huu wa kuokoa Maisha ya wananchi. Usambazaji wa chanjo hizi utaanza rasmi haraka siku ya Jumatano. Mpango huu utasaidia kuboresha afya za wananchi wetu. On

“Kuanzia Jumatano usambazaji utaanza kuelekea maeneo yote ya nchi. Na kwa kuanza itakua ni kwenye hospitali ya Juba, hospitali za jeshi na polisi. Amekaririwa Achuei akiongea na waandishi wa habari wakati wa mapokezi ya chanjo hizo kupitia uwanja wa ndege wa Juba International Airport Jumanne august 31..

Dr Fabian Ndenzako, muwakilishi wa shirika la afya duniani (WHO amesema “Napenda kutumia nafasi hii kushukuru msaada huu. Msaada huu wa chanjo utasaidia kwa kiasi kikubwa katika mapambano dhihi ya janga hili la Corona.

March mwaka huu Sudani Kusini ilipokea chanjo dozi 132,000 aiana ya AstraZeneca kutoka mpango wa Covax hata hivyo, mwezi May mwaka huu nchi ya Sudan Kusini ilizirejesha chanjo baada ya kudai kwamba haikua imejipanga kuanza kutoa huduma ya uchanjaji na hivyo ingepelekea kuharibika kwa chanjo hizo.

July 18 mwaka huu, baadhi ya maeneo ya Sudan Kusini yalitangaza kuharibika kwa dozi za chanjo ya AstraZeneca takribani 56,587.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live