Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan Kusini: Watu wenye silaha wavamia wanakijiji eneo lenye utajiri wa mafuta

Sudan Kusini: Watu Wenye Silaha Wavamia Wanakijiji Eneo Lenye Utajiri Wa Mafuta Sudan Kusini: Watu wenye silaha wavamia wanakijiji eneo lenye utajiri wa mafuta

Mon, 29 Jan 2024 Chanzo: bbc

Watu wenye silaha wamewashambulia wanakijiji katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Abyei linalozozaniwa na Sudan na Sudan Kusini, na kusababisha vifo vya takriban watu 52, akiwemo askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa, huku 64 wakijeruhiwa, afisa wa eneo hilo alisema Jumapili.

Sababu ya shambulio hilo Jumamosi jioni haikujulikana mara moja lakini inashukiwa kuzunguka mzozo wa ardhi, Bulis Koch, waziri wa habari wa Abyei, aliambia The Associated Press katika mahojiano ya simu kutoka Abyei.

Ghasia mbaya za kikabila zimekuwa za kawaida katika eneo hilo, ambapo wana kabila la Twic Dinka kutoka Jimbo jirani la Warrap wako katika mzozo wa ardhi na Ngok Dinka kutoka Abyei kuhusu eneo la Aneet, lililo mpakani.

Washambuliaji katika ghasia za Jumamosi walikuwa vijana wenye silaha kutoka kabila la Nuer ambao walihamia jimbo la Warrap mwaka jana kwa sababu ya mafuriko katika maeneo yao, Koch alisema.

Mzozo wa kijeshi wa Sudan unakaribia Sudan Kusini na Abyei, mjumbe wa Umoja wa Mataifa ameonya.

Katika taarifa yake, Kikosi cha Usalama cha Muda cha Umoja wa Mataifa cha Abyei (UNISFA) kimelaani ghasia hizo.

Sudan na Sudan Kusini zimetofautiana kuhusu udhibiti wa eneo la Abyei tangu makubaliano ya amani ya mwaka 2005 yalipomaliza miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya kaskazini na kusini mwa Sudan.

Sudan na Sudan Kusini zote zinadai umiliki wa Abyei, ambayo hadhi yake haikutatuliwa baada ya Sudan Kusini kuwa huru kutoka kwa Sudan mwaka 2011

Chanzo: bbc