Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan Kusini: Upinzani wapinga gharama fomu ya Urais

Sheria Ya Uchaguzi Ya Sudan Kusini Yawafanya Wabunge Kuandamana Sudan Kusini: Upinzani wapinga gharama fomu ya Urais

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchini Sudan Kusini, vyama vya upinzani vinapinga ongezeko kubwa la ada wanayotakiwa kulipia ili kujisajiliwa kama wagombea wa nafasi mbalimbali kuelekea uchaguzi wa mwezi Desemba mwaka huu ambapo sasa watalazimika kilipa dola za Marekani elfu 50.

Hatua hii inakuja wakati ambapo raia wa Sudan Kusini wanatarajiwa kushiriki uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia mwezi Desemba mwaka huu, uchaguzi ambao tayari upinzani unahoji kiwango cha tozo ya kuchukua fomu za kugombea.

Tangazo la kuvitaka vyama vya siasa kulipa Dolla elfu 50 kushiriki uchaguzi huo lilitolewa na kamati iliyopewa jukumu la kuratibu uchaguzi huo.

Awali vyama vya siasa vilitakiwa kulipia ada ya Dolla 150 huku kamati inayoratibu maandalizi ya uchaguzi huo ikikosa kutoa sababu za kuongeza ada.

Haya yanajiri wakati huu muungano wa vyama 14 vya upinzani ukishiriki maadamano kupinga hatua hiyo jijini Juba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live