Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan Kusini: UN yalaani mauaji ya afisa wake wa kulinda amani

Mauaji UN Maafisa Sudan.png Sudan Kusini: UN yalaani mauaji ya afisa wake wa kulinda amani

Wed, 6 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujumbe wa kulinda amani nchini Sudan Kusini (UNMISS) imelaani mauji ya mmoja wafanyikazi wake kwenye taifa hilo.

Charles Kiir Gone alikuwa akihudumu na ujumbe huo wa kulinda amani katika eneo la Wau Kaskazini Magharibi wa nchi hiyo.

Mhudumu huyo wa UN aliripotiwa kuuawa wakati wa shambulio la watu wenye silaha akiwa katika makazi ya jamaa wake ambapo alikuwa anaishi kabla ya kisa hicho kutokea.

Kwa mujibu wa kituo cha redio cha kibinafasi nchini Sudan Kusini, afisa huyo wa Umoja wa Mataifa aliuawa akiwa kwenye likizo, mauaji yake yakihusishwa na wizi wa mifugo.

UNMISS imetoa wito kwa mamlaka nchini Sudan Kusini kuanzisha uchunguzi dhidi ya mauaji ya afisa huyo na kuwaajibisha wahusika.

Sudan kusini imekuwa ikikabiliwa na changamoto wa wizi wa mifugo, maelfu ya raia wakiripotiwa kuuawa katika matukio yanayohusishwa na wizi huo wa mifugo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live