Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan Kusini: Njia ya kuelekea utulivu inakabiliwa na changamoto

Kiir Wa Sudan Kusini Aahidi Uchaguzi Wa Kwanza Nchini Humo Sudan Kusini: Njia ya kuelekea utulivu inakabiliwa na changamoto

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Njia ya Sudan Kusini kuelekea utulivu, ikiwa ni pamoja na kupata serikali mpya iliyochaguliwa na raia, inakabiliwa na changamoto wakati huu vita katika nchi jirani ya Sudan vikitishia kuelemea Juba, ambayo inakabiliwa na wimbi la wahamiaji pamoja na hali mbaya ya hewa.

Taarifa hii imetolewa wakati ambapo Tume ya Pamoja ya Ufuatiliaji na kufanya Tathmini ya mchakato wa amani nchini Sudan kusini, ambayo wiki hii ilifanya kumbukizi nyingine tangu kuanza kwa serikali ya mseto iliyoanzishwa na mkataba wa amani wa 2018 kati ya Rais Salva Kiir na makundi mbalimbali yenye silaha.

Akizungumza wakati wa sherehe za maadhimisho hayo, mwenyekiti wa tume hiyo Meja Jenerali Tai Gituai,alifahamisha kuwa sherehe hizo zilihusu zaidi kuorodhesha matatizo ambayo hayajatatuliwa badala ya mafanikio.

Ikiwa imesalia miezi kumi kabla ya kufanyika kwa uchaguzi nchini Sudan Kusini, Gituai alisema inatia wasiwasi kwamba mahitaji muhimu hayajakamilika, na hakuna maelewano kati ya vyama kuhusu uchaguzi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live