Kiongozi wa kikosi cha wanamgambo nchini Sudan cha RSF Mohamed Hamdan Daglo anatuhumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita nchini Sudan, wakati huu akiendeleza ziara yake kwa mataifa ya Kikanda, ziara inayondekana kuwagawa msimamo ya viongozi wa kikanda.
Hamdan Daglo amekua akifanya safari za kikanda ikiwa ni juhudi za kujaribu kujaribu kutafuta ungwaji mkono na viongozi wa kikanda na bara Afrika, kujaribu kusuluhisha mzozo ambao umepelekea vita kati ya kikosi chake cha RSF na jeshi la Sudan.
Kiongozi huyo wa RSF pia alizuru Afrika Kusini ambapo alikutana na rais Cyril Ramaphosa
Hamdan amefanya mazungmzo na marais wa Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Rwanda, na Djibouti pamoja na Ethiopia, ili kutafta njia mwafaka ya kumaliza mzozo na kwamba mchakato wa amani unaoendelezwa na IGAD, unastahili kufikia suluhu ya kisiasa itakayoleta amani ya kudumu nchini humo, ambapo kiongozi huyo anapata ungwaji mkono kutoka utawala wa Chad.
Naye kiongozi wa utawala wa kijeshi nchini Sudan Abdel Fattah Al-Burhan akionekana kupata ungwaji mkono kutoka kwa Misri na Eritrea.