Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Jeshi lazidisha mashambulizi kwa vikosi RSF

Sasa Si Wakati Wa Mazungumzo   Mkuu Wa Jeshi La Sudan Sudan: Jeshi lazidisha mashambulizi kwa vikosi RSF

Sun, 3 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vikosi vya Wanajeshi wa Sudan (SAF) vimezidisha mashambulizi ya anga na ya mizinga kwenye maeneo ya Kikosi cha Wanajeshi wa Msaada wa Haraka (RSF) katika mji mkuu wa nchi hiyo Khartoum.

Duru moja mjini Khartoum imeliambia shirika la habari la Xinhua kwamba ndege za kivita za jeshi la Sudan (SAF) zimeshambulia maeneo ya RSF ndani ya mji wa Omdurman na katika maeneo mengine ya kaskazini magharibi mwa Khartoum. Mashambulizi haya yamelenga vitongoji kama vile Ombada na Dar Al Salam vya magharibi mwa Omdurman pamoja na kitongoji cha Al Salha Kusini.

Duru hiyo imeongeza kuwa, jeshi la anga la Sudan pia limeanzisha mashambulizi kwenye vituo vya RSF katika kitongoji cha Al-Kadaro cha mji wa Bahri wa kaskazini mwa Khartoum.

Wahanaga wakuu wa vita vya majenerali wa kijeshi Sudan ni raia wa kawaida hasa watoto wadogo

Wakati huo huo, Mohamed Kandasha, msemaji wa Chumba cha Dharura cha eneo la Kusini mwa Khartoum, ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook siku ya Jumamosi kwamba jeshi la anga Sudan limefanya mashambulizi makali ya mabomu katika vitongoji vya Al-Inghaz, Al-Azhari na Al-Salama vya kusini mwa Khartoum.

"Vitongoji vya Khartoum Kusini vimekumbwa na mashambulizi ya anga na mizinga tangu asubuhi," Kandasha alisema na kuongeza kuwa, watu wawili wameuawa, na wengine kumi wamejeruhiwa baadhi yao wakiwa na hali mbayakutokana na shambulio lililoshwa kwenye eneo la makazi ya watu na la biashara karibu na Hospitali ya Razi katika kitongoji cha Al-Azhari.

Khartoum mji mkuu wa Sudan umegawika kwenye sehemu tatu kuu zinazotenganishwa na makutano ya mito ya Blue Nile na White Nile. Maeneo hayo yanaundwa miji inayojitegemea ambayo ni Khartoum, Omdurman, na Bahri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live