Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Jeshi laituhumu RSF kwa kuua raia wasio na hatia

Rsf Watuhumiwa Sudan: Jeshi laituhumu RSF kwa kuua raia wasio na hatia

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Sudan na makundi ya wananchi yamevishutumu Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kuwa vimeua makumi ya raia wasio na silaha katika majimbo ya Kordofan Kusini, Al-Jazirah na Sennar.

Makundi ya wananchi yanayoshrikiana na Jeshi la Serikali ya Sudan katika mji wa Al-Hasahisa, takriban kilomita 45 kaskazini mwa Wad Madani, mji mkuu wa Jimbo la Al-Jazirah (katikati), yamesema kuwa takriban raia 4 waliuawa na wapiganaji wa RSF wakati wa uvamizi wao kwenye vijiji vya mkoa wa Al-Hasahisa.

Taarifa iliyotolewa na makundi hayo imethibitisha kuwa Kikosi cha Msaada wa Haraka kimevamia vijiji vya Maryoud, Tanub na Futais kwa nia ya kupora na kusababisha vifo vya raia, japokuwa kuna ugumu wa kupata taarifa za ukiukwaji wa sheria uliofanywa na RSF kutokana na kukatika kwa mawasiliano ya mtandao katika jimbo la Al-Jazirah kwa siku 20 sasa.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, kuwa vitendo vya Kikosi cha Msaada wa Haraka vimewalazimisha wanawake, watoto, wazee na wagonjwa kukimbia makazi yao hadi mji wa El Manaqil, magharibi mwa Jimbo la Al-Jazirah, ambalo liko ndani ya maeneo yanayodhibitiwa na Jeshi la Sudan.

Katika muktadha huo huo, Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema kwamba "Vikosi vya Msaada wa Haraka vimezidisha mashambulizi dhidi ya raia, vijiji na miji salama katika maeneo tofauti ya nchi katika siku zilizopita." Mamilioni ya Wasudani wamekimbia makazi yao kutokana na vita

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imeongeza kuwa wiki hii, "magenge ya wanamgambo wahalifu" (RSF) yalishambulia idadi kadhaa ya vijiji vya Jimbo la Kordofan Kusini na kuteketeza vijiji 5, kuua zaidi ya wanakijiji 60 wasio na silaha, na kuteka nyara wengine.

Haya yanajiri huku vita vya kuwania madaraka vikiendelea kuchachamaa nchini Sudan. Juhudi za kieneo na kimataifa za kuzishawishi pande mbili hasimu kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kutatua tofauti zao hazijafua dafu mpaka sasa.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA), watu zaidi ya 13,000 wameuawa tangu mapigano baina ya pande hizo mbali yaanze nchini Sudan katikati ya Aprili mwaka uliopita 2023.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live