Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Jeshi lachukua tena makao makuu ya shirika la utangazaji

Sudan: Jeshi Lachukua Tena Makao Makuu Ya Shirika La Utangazaji Sudan: Jeshi lachukua tena makao makuu ya shirika la utangazaji

Wed, 13 Mar 2024 Chanzo: Bbc

Wanajeshi kutoka jeshi la Sudan wameteka tena makao makuu ya shirika la utangazaji la serikali huko Omdurman, mji ulio ng'ambo ya Mto Nile kutoka mji mkuu, Khartoum, jeshi limesema.

Haya ni mafanikio ya kiishara kwa jeshi katika vita vyake vya wenyewe kwa wenyewe vya miezi 11 na Vikosi vya Rapid Support Forces (RSF).

RSF ilikuwa imeshikilia makao makuu tangu tu baada ya mapigano kuzuka.

Mzozo wa Sudan umesababisha watu milioni nane kukimbia makazi yao na kuna onyo la kuongezeka kwa njaa.

Video zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanajeshi wakisherehekea nje ya kituo cha utangazaji cha serikali huko Omdurman.

Katika taarifa, jeshi liliita hatua hiyo "ushindi mkubwa".

Lakini licha ya kuchukua jengo hilo Aprili mwaka jana, RSF haikuweza kutangaza kutoka humo na televisheni ya taifa iliendelea kuonyesha maudhui yanayounga mkono jeshi, ambayo yalitangazwa kutoka mahali pengine nchini.

Tangu vita vilipoanza, jeshi na RSF wamepigania udhibiti wa Khartoum na miji ya karibu. Licha ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutoa wito wa kusitishwa kwa mapigano katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, mapigano makali yameendelea katika maeneo kadhaa ya mji mkuu.

"Watu wamefurahia sana - kuna hisia nyingi kwenye redio ya taifa," anasema mwandishi wa BBC Mohanad Hashim ambaye hapo awali alifanya kazi katika shirika la utangazaji la serikali ya Sudan.

"Pia ni kushindwa sana kwa RSF kwa sababu walikuwa wakitumia kituo cha redio cha HQ kama ngome yao. Vikosi vya Wanajeshi vya Sudan vinaenda kumaliza hili - ni ushindi mkubwa kwao."

Mzozo huo ulizuka mwezi Aprili uliopita kufuatia kutoelewana kati ya mkuu wa jeshi, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, na mkuu wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, anayejulikana zaidi kama Hemedti, kuhusu mpango wa kisiasa unaoungwa mkono kimataifa kuelekea utawala wa kiraia.

Pamoja na kuwahamisha mamilioni ya watu, mzozo huo umeiacha Khartoum kuwa magofu, na kusababisha mgogoro wa kibinadamu na mauaji yaliyochochewa kikabila huko Darfur, magharibi mwa nchi hiyo.

Majaribio kadhaa ya kimataifa ya kufikiwa kwa makubaliano ya usitishaji mapigano yameshindwa.

Chanzo: Bbc