Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Jeshi la Sudan lasema wanajeshi 177 wa Misri wameokolewa

Sudan: Jeshi La Sudan Lasema Wanajeshi 177 Wa Misri Wameokolewa Sudan: Jeshi la Sudan lasema wanajeshi 177 wa Misri wameokolewa

Thu, 20 Apr 2023 Chanzo: Bbc

Jeshi la Sudan linasema kuwa Wanajeshi 177 wa Misri, ambao walikuwa wamekamatwa na kikundi cha jeshi wameokolewa Jumatano.

Kikundi hicho kilisafirishwa kwa ndege nje ya Sudan kwa ndege nne za kijeshi la Misri.

Wakiliwa wamekamatwa na kikundi cha kijeshi cha RSF Jumamosi walipokuwa katika mazoezi ya pamoja ya kijeshi na jeshi la Sudan.

TJeshi la Misri halikutangazakuhusu uokoaji huo – lakini awali lilisema kuwa linashirikiana na mamlaka za Sudan ili kuwawezesha wanajeshi hao kurejea nyumbani.

Nchi kadhaa zikiwemo Japan na Tanzania zimetangaza kuwa zingependa kuwaondosha raia wake , lakini mapigano nchini Sudan yamechelewesha mipango yao.

Wanadiplomasia wa kigeni wamekuwa wakishambuliwa na baadhi ya wafanyakazi wa misaada wameripotiwa kuwa waathiriwa wa ghasia.

Chanzo: Bbc