Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Hospitali zaripotiwa kuwa na uhaba wa dawa, watumishi

C2375ABA B7AF 47DF B011 7549A079982E.jpeg Sudan: Hospitali zaripotiwa kuwa na uhaba wa dawa, watumishi

Sun, 30 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Madaktari wanaofanya kazi katika hospitali ya Al-Now huko Omdurman Sudan inalalamikia ukosefu vifaa tiba na dawa katika kipindi hiki cha vita vinavyoendelea nchini humo.

Taarifa ya jumuiya hiyo imesema kuwa, idadi ndogo ya madaktari na wauguzi wanahangaika kuhudumia wimbi la wagonjwa wanaofika hapo kwa ajili ya matibabu.

Dakta Alaa Mohammed, tabibu katika hospitali ya Al-Now huko Omdurman anasema kwa sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa timu za madaktari na vifaa tiba. Amesema kwa kawaida kunawepo timu mbalimbali za madaktari lakini wakati huu Sudan iko vitani zamu za madaktari na wauguzi zinakuwa ndefu kutokana na uhaba wa wafanyakazi. Daktari huyo amesema daktari mmoja tu anafanya kazi katika idara mbili au tatu wakati mwingine.

Kuendelea mapigano Sudan Wakati huo huo watu waliojitolea kufanya kazi katika hospitali hiyo ya Omdurman wamesema hakuna mafuta kwa ajili ya magari ya kubebea wagonjwa huku kitengo cha huduma ya Dialysis kwa wagonjwa wa matatizo ya figo kikisalia bila vifaa.

pande mbili za jeshi zinazopigana nchini Sudan zimeendelea kukiuka makubakliano ya tano ya kusitisha vita huku mapigano makali yakiendelea kuripotiwa katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu, Khartoum.

Ripoti zinasema kuwa mapigano makali ya silaha nzito kati ya jeshi la Sudan na Vikosi vya Radiamali ya Haraka (RSF) yameendelea leo kaaribu na Kamandi ya Jeshi na Ikulu ya Rais mjini Khartoum.

Wizara ya Afya ya Sudan imetangaza kuwa hadi sasa watu wasiopungua 512 wakiwemo raia wa kawaida na askari jeshi wameuawa tangu tarehe 15 mwezi huu na wengine 4,200 wamejeruhiwa katika mapigano yaliyoanza Sudan mwezi huu wa Aprili.

Wakati huo huo Shirika la Habari la Ufaransa lilisema kuwa idadi ya waliouawa kutokana na mapigano yaliyoibuka huko Darfur, Magharibi mwa Sudan, imeongezeka hadi 574, baada ya watu 74 kuuawa jana Ijumaa katika mji wa El Geneina.

Mapigano ya kikabila yaliibuka huko Darfur baada ya kuzuka vita kati ya wapiganaji wa RSF na jeshi la Sudan zaidi ya wiki mbili zilizopita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live