Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sudan: Hakuna utatuzi wa kisiasa mpaka uasi uishe

 Mkuu Wa Jeshi La Sudan Aelekea Misri Safari Ya Kwanza Tangu Aprili Sudan: Hakuna utatuzi wa kisiasa mpaka uasi uishe

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, kamanda mkuu wa Jeshi la Sudan (SAF), amesema kuwa, hakuna mchakato wa kisiasa unaoweza kufanyika nchini Sudan maadamu waasi wanaendelea kupigana na jeshi la nchi hiyo na hali hiyo itaendelea hadi pamoja uasi huo utakapokomeshwa.

Jenerali Al-Burhan, ambaye pia anaongoza Baraza la Mpito la Utawala la Sudan, amesema hayo wakati akiwahutubia wanajeshi kwenye kambi ya kijeshi ya Blue Nile katikati mwa mji wa Sennar.

Vile vile ameelezea azma ya jeshi la Sudan ya kukomesha uasi na kuruhusu watu kurejea makwao na kudai kuwa, dalili za ushindi zimeanza kujitokeza.

Uchu wa madaraka baina ya najenerali wa kijeshi umeitumbukiza Sudan kwenye mapigano ya maangamizi tangu tarehe 15 Aprili 2023 na hakuna dalili zozote za kumalizika maafa ya wananchi wa nchi hiyo ya Kiarabu ya barani Afrika. Wahanga wakuu wa vita vya uchu wa madaraka baina ya majenerali wa kijeshi Sudan, ni raia wa kawaida

Ugomvi baina ya majenerali wa kijeshi nchini Sudan umezusha mapigano makali kati ya jeshi SAF na Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF na hadi hivi sasa yameshasababisha maelfu ya watu kuuawa na mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.

Ofisi ya Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ilisema wiki iliyopita kuwa, zaidi ya watu 13,000 wameshauawa na zaidi ya milioni 9 wamekimbia makazi yao tangu mapigano yalipoanza baina ya majenerali hao wa kijeshi nchini Sudan, tarehe 15 Aprili, 2023.

Wiki hii, mwakilishi wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema kuwa, vita vya uchu wa madaraka baina ya majenerali nchini Sudan vinahatarisha mustakabali wa raia milioni 24 wenye umri mdogo zaidi wa nchi hiyo.

Mandeep O’Brien aliyasema hayo na kuongeza kuwa, Sudan inakabiliwa na janga kubwa la kibinadamu lisiloelezeka. "Ni jinamizi lililo hai kwa watoto" alisema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live