Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Straika Platinum aihofia Simba

Straika Pic Data Straika Platinum aihofia Simba

Sat, 9 Jan 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Mwandishi WetuMore by this Author Licha ya timu yake kuwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 ilioupata nyumbani, mshambuliaji wa FC Platinum, Silas Songani amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya ili kuitupa nje Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Songani hakucheza katika mchezo wa kwanza jijini Harare kutokana na majeruhi ni miongoni mwa nyota 23 walio katika msafara wa timu hiyo ambayo itakutana na Simba katika mchezo wa marudiano utakaochezwa kuanzia saa 11 jioni katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini.

Songani alisema licha ya timu yake kuwa na faida ya ushindi wa nyumbani, katika mechi ya marudiano keshokutwa Jumatano wanahitajika kupambana kwa hali na mali.

"Tulipata matokeo mazuri dhidi ya Simba  lakini fundo moja halitoshi kusaidia kwenye kiangazi. Tunatakiwa kuwamaliza Simba. 

Tuna kazi kubwa mbele yetu lakini uaminifu, uadilifu, kujituma na utayari wa kusonga mbele ni chachu kwetu kusonga mbele.

Kinachonivutia zaidi kwa hili kundi ni kiu ya kufanya mazoezi kwa bidii na kila mchezaji anapambana ili apate nafasi kwenye timu," alisema Songani.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz