Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stephen Curry arejea uwanjani NBA, timu yake yafungwa tena

98191 Pic+nba Stephen Curry arejea uwanjani NBA, timu yake yafungwa tena

Fri, 6 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Norm Powell alifunga pointi 37, ambazo ni nyingi kwake tangu aanze kucheza, wakati mabingwa wa Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA), wakati Toronto Raptors walipotibua kurejea uwanjani kwa Stephen Curry, baada ya kupata ushindi wa pointi 121-113 dhidi ya Golden State jana Alhamisi na hivyo kupata nafasi ya kucheza hatua ya mtoano kwa msimu wa saba mfululizo. Baada ya kutoonekana uwanjani kwa miezi minne kutokana na kuvunjika mkono, Curry alirejea katika kikosi cha Warriors kilipokutana na Toronto kw amara ya kwanza tangu kumalizika kwa fainali za NBA. "Tulijua kuwa Steph angekuwa uwanjani kwa hiyo ingekuwa usiku mzuri na mazingira mazuri," alisema nyota wa Raptors, Kyle Lowry. "Ni mmoja wa wachezaji bora katika ligi kw ahiyo ilitulazimu kuwa makini na kumchunga." Baada ya kuanza taratibu, Curry alimaliza mechi hiyo akiwa ameifungia pointi 23 timu ya Warriors ambayo inakosa wachezaji wengi kutokana na kuwa majeruhi. Warriors imeshinda michezo 14 tu msimu huu na ndiyo yenye rekodi mbaya katika ligi. "Nilijisikia vizuri. Ulikuwa wakati mtulivu na uliokuwa na msisimko kadri mchezo ulivyokwenda. Toronto ni timu ya ubingwa kwa hiyo wana muunganiko mzuri sehemu nyingi," alisema Curry, ambaye amekosa mechi 58. Msimu huu wanamkosa pia Klay Thompson, ambaye aliumia goti katika mechi aliyofunga pointi 30 dhidi ya Toronto. Warriors sasa imeshinda michezo miwili kati ya minne iliyopita baada ya kupoteza michezo nane mfululizo. Pia wamepoteza mechi 10 mfululizo nyumbani na inasubiriwa kuona kama Curry anaweza kuiokoa timu kutoka katika kiwango kibovu msimu huu.

Chanzo: mwananchi.co.tz