Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Stars yaiendea Tunisia Uturuki

30054677036afdb7cd5014e719134f19 Stars yaiendea Tunisia Uturuki

Sun, 8 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KIKOSI cha timu ya soka ya taifa, Taifa Stars kimeondoka Alfajiri ya leo kwenda Uturuki kwa maandalizi dhidi ya mechi ya Tunisia huku kocha wake Ettiene Ndayiragije akitamba kufuata dawa ya ‘kuwaua’ wapinzani wao.

Stars inatarajiwa kucheza na Tunisia Novemba 13 mjini Tunis katika mechi ya kuwania kufuzu michuano ya kombe la mataifa Afrika, Afcon.

Akizungumza na gazeti hili saa chache kabla ya kuondoka,Ndayiregije alisema wanaondoka wakiwa na lengo moja la kufanya vyema katika mchezo wao.

Akizungumza na gazeti hili jana, Ndayiragije alisema amewafuatilia wapinzani wao kwa muda mrefu na timu yake itaingia uwanjani ikifahamu ubora na mapungufu ya wenyeji wao.

Ndayiragije alisema alikuwa na mawasiliano ya karibu na wachezaji wake wote aliowaita, hivyo maandalizi ya kuwakabili Tunisia ameyafanya kwa muda mrefu.

"Tunaondoka usiku wa kuamkia kesho (Alfajiri ya leo), tuko vizuri, tunaenda huko kwa kazi moja ya kupambana, naamini mechi itakuwa nzuri, ninawaandalia 'surprise'," alisema Ndayiragije.

Alisema, anahitaji kupata ushindi ili akae kwenye nafasi nzuri katika kundi lao na kamwe haendi kutafuta matokeo mengine.

"Tunazihitaji pointi tatu, ndio maana ninasema tunakwenda kuwashangaza," alisema.

Alisema anaamini kila mchezaji aliyemwita atatoa mchango mkubwa kwenye timu kwa sababu wote 'wanasafiri njia moja' katika michuano hiyo.

Baada ya mechi hiyo ya kwanza, Taifa Stars inayoongozwa na nahodha, Mbwana Samatta, itarejea nchini mapema ili kuwakabili wapinzani wao kwenye uwanja wa Mkapa Novemba 17.

Katika mechi ya kwanza ya Kundi J, Stars ilikubali kichapo cha mabao 2-1dhidi ya Libya, mchezo ambao ulichezwa mjini Tunis pia.

Chanzo: habarileo.co.tz