Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spurs ya Mourinho yachezea kichapo kwa Leipzig

98653 Pic+mou Spurs ya Mourinho yachezea kichapo kwa Leipzig

Wed, 11 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

London, England. Kocha wa Tottenham Spurs, José Mourinho amesema kikosi chake kinawakati mgumu msimu ujao kushiriki  katika Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuondolewa na RB Leipzig ya Ujerumani kwa jumla ya mabao 4-0.

Spurs katika mchezo wa kwanza nchini England walipoteza kwa bao 1-0, walishindwa kufua dafu  katika mchezo wa marudiano mbele ya Leipzig kwa kukubali kipigo cha mabao 3-0  kwenye uwanja wa Red Bull Arena.

“Kwa kikosi nilichonacho katika kipindi hiki ni ngumu mno,” alisema Mourinho. “Kibaya zaidi ni kwamba tatizo letu haliwezi kumalizika leo wala kesho, lakini tutapambana hadi mwisho.

“Upande wa Ligi Kuu England tumekuwa tukipata matokeo tofauti na yale ambayo tumekuwa tukiyahitaji. Tumepoteza 3-2, 2-1, 1-0 haina maana kuwa hatotoendelee kupambana,” alisema kocha huyo mwenye maneno mengi.

Spurs katika michezo iliyopita iliwakosa wachezaji wao muhimu wakiwemo, Steven Bergwijn, Ben Davies, Harry Kane, Davinson Sánchez, Moussa Sissoko na Son Heung-min kutokana na kusumbuliwa kwao na majeruhi.

“Nadhani wapinzani wetu walistahili kuingia nane bora kutokana na  kikosi change kusumbuliwa na majeruhi wengi. Hakuna timu ambayo inaweza kukosa wachezaji wake watano hadi sita alafu ikaendelea kufanya vizuri ni lazima wapungue makali,” alisema.

Pia Soma

Advertisement
 Mourinho alitoa kali katika mahojiano yake baada ya kusema  kwa mazingira ya kikosi chake kilivyo basi wachezaji wa akiba wa Leipzig wanaweza kupata namba ya kucheza kwenye kikosi chake cha kwanza bila tatizo lolote.

Chanzo: mwananchi.co.tz