Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika wa bunge la Afrika Kusini ajisalimisha polisi

Spika Wa Bunge La Afrika Kusini Ajisalimisha Polisi Spika wa bunge la Afrika Kusini ajisalimisha polisi

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Spika wa Bunge la Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula amejisalimisha kwa polisi siku moja baada ya kujiuzulu kwa tuhuma za rushwa.

Bi Mapisa-Nqakula alifika katika kituo cha polisi huko Centurion, kilomita 40 kutoka Johannesburg siku ya Alhamisi.

Anatarajiwa kufika kortini kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Pretoria kwa tuhuma za ufisadi.

Mwanasiasa huyo anatuhumiwa kuomba hongo ili kurudisha kandarasi wakati alipokuwa waziri wa ulinzi.

Baada ya wiki kadhaa za uchunguzi, Bi Mapisa-Nqakula alijiuzulu siku ya Jumatano, akisema hatua hiyo haikuwa "ishara au kukubali hatia".

Alisema kutokana na "uzito" wa uchunguzi hawezi kuendelea na jukumu lake.

Hapo awali alikana kosa lolote.

Chanzo: Bbc