Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika wa Somalia alaani vikali shambulio kwenye kambi ya jeshi

Shambulio Kambi Ya Jeshi Spika wa Somalia alaani vikali shambulio kwenye kambi ya jeshi

Wed, 26 Jul 2023 Chanzo: Voa

Spika wa bunge la Somalia amelaani vikali shambulio la Jumatatu la woga lisilo na huruma na lisilo na utu au kumuogopa Mungu katika kambi ya kijeshi lililouwa wanajeshi 25 na kujeruhi wengine zaidi ya 70.

Sheik Adan Mohamed Nur, maarufu kama Adan Madobe, amesema anashuku wasaliti wanaweza kuwa walifanikisha shambulio hilo la bomu.

Najua kati ya maafisa wa Polisi wako ambao ni wazuri, wachapa kazi na wenye heshima lakini wasaliti wamewezesha hili. Ninashuku hilo sana. Haivumiliki alisema kwenye video iliyowekwa na vyombo vya habari vya serikali.

Kundi la wanamgambo wa al-Shabab lilidai kuhusika na shambulio hilo. Katika taarifa kwenye mtandao wa Telegram, al-Shabab ilisema mmoja wa washambuliaji wake wa kujitoa muhanga ndiye aliyetekeleza shambulio hilo.

Chanzo: Voa