Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spika wa Bunge Afrika Kusini asomewa Mashtaka 12 ya Ufisadi

Nosiviwe Mapisa Nqakula.jpeg Spika wa zamani wa Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Spika wa zamani wa Afrika Kusini Nosiviwe Mapisa-Nqakula ameshtakiwa na makosa 12 ya ufisadi na moja la utakatishaji fedha.

Alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi baada ya kujisalimisha polisi saa za asubuhi.

Mwanasiasa hyo anatuhumiwa kwa kudai rushwa ili atoe mikataba wakati akiwa waziri wa ulinzi.

Alikanusha kufanya makosa yoyote mahakamani akisema: “Sina tabia ya kufanya uhalifu.”

Lakini mwendesha mashtaka Bheki Manyati ameiambia mahakama ya mwanzo ya Pretoria kuwa kuna “ushahidi wa kutosha” dhidi ya Bi Mapisa-Nqakula.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live