Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Spiderman ageuka mzoa taka

Spiderman Taka.png Jonathan Olakunle almaarufu Spiderman wa Nigeria akifanya usafi katika mitaa ya sokoni

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KAMA wewe ni mtumiaji wa mitandao ya kijamii, bila shaka utakuwa umeshakutana na video zinazomuonesha ‘Spiderman wa mchongo’ anayecheza Taarab kwa kukata viuno kwenye mitaa mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam na kutoa burudani kwa wengi.

Sasa achana na huyo, Jonathan Olakunle almaarufu Spiderman wa Nigeria, naye anazunguka mitaani akiwa ndani ya mavazi hayo yaliyopata umaarufu kupitia filamu za ‘spiderman’ lakini tofauti na yule wa Bongo, huyu anafanya jambo la maana zaidi!

Jamaa anazunguka kwenye mitaa mbalimbali ya Mji wa Osogbo katika Jimbo la Osun nchini Nigeria akiokota taka zilizotupwa hovyo mitaani lakini pia akitoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi.

Olankule ambaye ni mwanaharakati wa utunzaji wa mazingira, amekuwa akipita kwenye masoko, kwenye mitaro ya maji machafu, mitaani na mahali popote palipo na taka ambapo kazi yake kubwa ni kuzikusanya na kwenda kuzitupa sehemu sahihi ikiwa ni pamoja na kwenye mapipa ya taka na kwenye madampo.

“Kila sehemu katika nchi ya Nigeria inahitaji mtu kama mimi, mimi ndiyo Spiderman wa Nigeria,” alisema Olankule alipohojiwa na Shirika la Habari la BBC na kueleza kwamba anaamini kama kila mtu atatekeleza majukumu yake ya kutrupa taka sehemu sahihi na kuzihifadhi, mitaa itakuwa misafi na kulinda afya za wananchi.

“Sifurahishwi na namna taka zinavyotupwa kila mahali, imeshakuwa sehemu ya kawaida ya maisha yetu kutupa taka hovyo kila mahali wakati haitakiwi kuwa hivi.

“Nilianza kusafisha mazingira mwaka 2004, nayachukiamazingira machafu na siku zote nilikuwa najisikia raha kufanya usafi kwenye mazingira ya nyumbani kwangu. Siku moja niliamua kuingia mtaani na kufanya usafi kama ninavyofanya kwenye mazuingira yangu na hapo ndipo safari ilipoanzia,” alisema Olankule.

Kuhusu aina ya mavazi anayoyatumia, Olankule anasema aliamua kuchagua vazi la Spiderman ili kuwavutia watu ambao wangeanza kumtazama kama shujaa wa mazingira kama inavyotokea kwa sasa.

Anaeleza kwamba awali wakati anaanza kazi hiyo, alikuwa akipata ugumu kuwashawishi watu wengine wafanye naye usafi kwenye mazingira yao ndipo alipoamua kuja na wazo la kibunifu la kuvaa mavazi ya Spiderman ambayo humfanya kuwa kivutio na hata anapowashawishi watu wakubali kushirikiana naye, wamekuwa wakifanya hivyo tofauti na mwanzo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live