Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sonko aunga mkono Ruto kuwafadhili makahaba

0fgjhs3pjqp3ffdsug Sonko aunga mkono Ruto kuwafadhili makahaba

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko amekiri kwamba kwa wakati mmoja aliwahikuwa mteja wa wafanyabiashara wa ngono kabla ya kumuoa mke wake Primerose Mbuvi.

Kupitia kwenye video alizopakia kwenye mitandao ya kijamii, Sonko alisema kwamba haona dosari yotote naibu Rais William Ruto akiwafadhili wafanyakazi wa ngono kwa sababu wengine wao wanakimu maisha kutokana na biashara hiyo.

Kulingana na Sonko, wanawake wanajihusisha na biashara hiyo kwa ajili ya hali ngumu ya kiuchumi nchini.

" Kuna changamoto nyingi sana jijini Nairobi, mimi huona watu wengi wanawatusi na kuwakashifu wafanyabiashara wa ngono ilihali ni wateja wao. Pia mimi nilikuwa mteja wao mkubwa sana kabla nimuoe mke wangu Primerose, sioni kama kuna jambo mbaya hapo, Mungu ni kila kitu." Tunajua wengi wao wanafanya hivyo kwa ajili ya kukimu maisha yao, naamini kamba wangekuwa wanajiweza, hawangefanya aina hiyo ya biashara." Sonko alisema.

Akijibu ombi la Ruto la kuwafadhili wafanyabiasha wa Ngono KSh milioni moja, Sonko alisema akwamba pia naye angewafadhili iwapo angekuwa amevalia kiatu cha Ruto.

Ruto ambaye anaazimia kumridhi Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi mkuu wa 2022 alisema kwamba yuko tayari kuwasaidi wananchi ambao hawajiwezi.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke