Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sonko aondolewa Ugavana wa Nairobi

Mike Sonko1 E1547036821112 660x400 Sonko aondolewa Ugavana wa Nairobi

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: millardayo.com

Bunge la Seneti limemuondoa Madarakani Gavana wa Nairobi, Mike Sonko, baada ya Maseneta 27 kupiga Kura za Ndio kuunga mkono kuondolewa kwake wakidai amekiuka Misingi ya Katiba, kutumia Ofisi vibaya na amekosa uwezo wa kuiongoza Nairobi.

Kuondolewa kwa Sonko kumetoa nafasi kwa Spika wa Bunge la Kaunti ya Nairobi, Ben Mutura kushikilia wadhifa huo hadi Uchaguzi wa Gavana na Naibu wake utakapofanyika katika kipindi cha siku 60 zijazo.

Aidha, Maafisa wa Magereza Nchini Kenya hivi karibuni walimshtaki kwa kutoroka jela miaka 20 iliyopita ambapo Bwana Sonko amekiri hadharani kutoroka jela wakati huo.

SABAYA AMBANANISHA KIGOGO WA SERIKALI ALIECHUKUA HELA ZA WALIMU, WANATOA MAMILIONI HAZIRUDI

Chanzo: millardayo.com