Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sonko amsaidia mtoto na mama yake waliokuwa wakiuza biskuti usiku

Sonko Amsaidia Mtoto Na Mama Yake Waliokuwa Wakiuza Biskuti Usiku Sonko amsaidia mtoto na mama yake waliokuwa wakiuza biskuti usiku

Fri, 23 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gavana wa zamani wa Nairobi Mike Sonko amemsaidia mama na mtoto wake waliokuwa wakiuza biskuti usiku katika barabara ya Hurlingham.

Katika video aliyopakia kwenye akaunti yake ya Twitter, Mike Sonko alimlipia salio la karo na kuahidi kufuatilia kesi hiyo na kumtafutia mama huyo kazi ya heshima ambayo haitahatarisha maisha yake.

Kulingana na Sonko alipatana na mtoto huyo takriban saa tatu na dakika 37 usiku wa Alhamisi na hadithi ya mama na mtoto huyo alimhurumisha sana na ikamlazimu kuingilia kati kuweza kuwasaidia.

“Majira ya saa 9.37 alasiri nikiwa round zangu mwenda pale kituo cha petroli huko hurligam, nilikutana na kisa cha kusikitisha na kuhuzunisha cha mama na bintiye mdogo Mariam wakiuza biskuti. Mama huyo alinijulisha kuwa anafanya kazi kwenye baridi ili kutafuta hela za kuwapea watoto wake maisha mema.”

Mtoto huyo alionekana akimuomba Sonko kununua biskuti hizo ambazo mama yake alikuwa akizitayarisha nyumbani.

Mama huyo alimwelezea kuwa alikuwa na shilingi elfu 7 ambazo alihitajika kulipa katika shule ambayo binti wake alikuwa akisoma na kuwa alikuwa akijaribu tu kumtafutia pesa hizo.

Mama huyo ambaye mume wake anaishi Mombasa alisema kuwa alikuwa akisafiri kutoka Kahawa West aliyoko katika barabara ya Thika hadi upande wa Hurlingham ili kuweza kujitafutia chakula cha kila siku.

Hii si mara ya kwanza mwanasiasa huyo kujitolea kuwasaidia watu wasiojiweza nchini.

Ikumbukwe wiki chache tu, Sonko alimwajiri bondia Conjestina kama mmoja wa walinzi wake na ata kuanda mbali zaidi nakuiandika familia nzima ya bondia huyo.

Miezi michache iliyopita, Sonko alimsaidia mwanafunzi mmoja kutoka kaunti ya Narok ambaye alikuwa akivalia sare ya shule iliyochanika.

Vitendo vya Sonko vya kuwasaidia msakini na wanyonge kumewaguza mioyo Wakenya na wanamitandoa wengi. Wanamitandaowalimshukuru na kumpongeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live