Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somo la haki za binadamu kufundishwa Malawi

9a0d4f7eb3e4a6487529374bf8a2ed13 Somo la haki za binadamu kufundishwa Malawi

Mon, 14 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

RAIS wa Malawi Lazarus Chakwera ametangaza nia na mipango ya serikali yake ya kuanzisha somo mahususi shuleni kwa ajili ya kuwafundisha watoto kuhusu Haki za Binadamu nchini humo.

Aidha kiongozi huyo ameagiza vyombo mbalimbali vya kusimamia haki na maisha ya wananchi vihakikishe kuwa adhabu kali inatolewa dhidi ya wale wanaofanya unyanyasaji wa kijinsia katika taifa hilo.

Rais Chakwera aliyasema hayo jana kutokana na taarifa iliyowasilishwa kwake iliyoonesha kuongezeka kwa kesi za udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia wakati wa janga la corona.

Katika hotuba yake kwa wananchi wa Malawi na Taifa kwa ujumla katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya Haki za Binadamu wikiendi hii, Chakwera alisema Malawi pia itahitaji kufundishwa kwa haki za binadamu mashuleni ili kuhakikisha kuwa wananchi wanaelewa vya kutosha kuhusu haki zao.

Rais Chakwera alisema takwimu inayoonyeshwa na idara ya taifa ya takwimu za ghasia za kijinsia inaogopesha.

“Miaka mitatu iliyopita, Ofisi ya Taifa ya Takwimu iliripoti kwamba mmoja kati ya wanawake na wasichana watatu wa Malawi kati ya miaka 15 hadi 49 anapata unyanyasaji wa kingono au kimwili,” Aliongeza Chakwera.

Chakwera alisema mwelekeo huo unaonyesha kuwa chini ya vizuizi vya kutoka vilivyowekwa ili kupambana na COVID-19, uhalifu wa kijinsia umeenea. Alitangaza mipango ya adhabu kali dhidi ya wale wanaofanya dhulma za kijinsia.

“Wizara za Sheria, Jinsia na utawala zitaandaa marekebisho ya sheria husika ikiwa ni pamoja na Utaratibu wa Makosa ya Jinai na nambari ya Ushahidi ili kuharakisha kushughulikiwa kwa kesi kama hizo, kutoa adhabu kali za lazima dhidi ya wakosaji na kuanzisha sajili ya wahalifu wa kijinsia.” alisema Chakwera.

Chanzo: habarileo.co.tz