Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somaliland yathibitisha ugunduzi wa mafuta

Somaliland Yathibitisha Ugunduzi Wa Mafuta Somaliland yathibitisha ugunduzi wa mafuta

Mon, 9 Jan 2023 Chanzo: Bbc

Jamhuri iliyojitangaza ya Somaliland imetangaza kugunduliwa kwa kisima cha mafuta katika eneo la Salhayey eneo la Marodi-Jeh, wizara yake ya nishati na rasilimali za madini ilisema katika taarifa iliyotumwa kwenye Facebook jana.

Wizara hiyo ilisema kuwa imeanzisha uchunguzi wa kisayansi baada ya kimiminika cheusi kumwagika kutoka kwenye eneo la kuchimba visima vya maji katika eneo hilo, na matokeo yamethibitisha kupatikana kwa mafuta.

Huu ni ugunduzi wa kwanza wa mafuta nchini Somalia. Taarifa hiyo iliongeza kuwa kampuni ya Uingereza ya Genel Energy itaanza utafutaji na uzalishaji zaidi wa mafuta.

Ugunduzi huo unakuja wiki mbili baada ya serikali ya shirikisho ya Somalia kuionya Genel Energy dhidi ya utafiti wa mafuta huko Somaliland bila idhini kutoka Mogadishu, ikisema kuwa kampuni hiyo inahujumu uhuru wake.

Somaliland, ambayo ilitangaza uhuru wake kutoka kusini mwaka 1991 na tangu wakati huo imekuwa ikitafuta kutambuliwa kimataifa bila mafanikio, ilisema kauli hiyo kutoka Mogadishu haina maana yoyote.

Chanzo: Bbc