Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somaliland yaapuuzilia mbali pendekezo la Uganda kuungana na Somalia

Somaliland Yaapuuzilia Mbali Somaliland yaapuuzilia mbali pendekezo la Uganda kuungana na Somalia

Mon, 25 Sep 2023 Chanzo: Bbc

Somaliland imesema "haina mpango wa mazungumzo kujadili umoja" baada ya Rais wa Uganda Yoweri Museveni kutoa pendekezo la kuwa mpatanishi kati ya nchi inayojiita jamhuri na serikali ya shirikisho ya Somalia.

Rais Museveni siku ya Jumamosi alisema "amekubali kuchukua jukumu la mratibu wa amani kati maeneo hayo mawili " baada ya kukutana na mjumbe wa serikali ya Somaliland katika mji wa Entebbe nchini Uganda.

Alisema Uganda haikuunga mkono kujitenga kwa jamhuri ya Somaliland "kwa sababu kimkakati, ni makosa".

Lakini katika taarifa,wizara ya mambo ya nje ya Somaliland ilisema kuwa mazungumzo yoyote na serikali mjini Mogadishu"haitajadili umoja, lakini jinsi nchi mbili zilizoungana hapo awali zinaweza kusonga mbele kila moja kwa njia tofauti".

"Kwa hiyo, Jamhuri ya Somaliland kwa mara nyingine tena inathibitisha kwa Umoja wa Afrika na jumuiya nyingine ya kimataifa kwamba haina mpango wa mazungumzo ya kujadili umoja na Somalia", iliongeza.

Somaliland ilijitangazia uhuru wake kutoka kwa Somalia mwaka 1991 na tangu wakati huo imekuwa ikitafuta kutambuliwa kimataifa bila mafanikio.

Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yamekuwa yakiendelea kwa miaka, na majadiliano kuanzia usimamizi wa anga na harakati za kuvuka mpaka hadi mahitaji ya Somaliland ya kutambuliwa kama nchi huru.

Chanzo: Bbc