Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia yawa mwanachama EAC

Somalia Mwanachamaa EAC (600 X 384) Somalia yawa mwanachama EAC

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taifa la Somalia sasa ni Mwanachama kamili wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) baada ya kukamilisha hatua zote zinazohitajika ili kuidhinishwa kuwa Mwanachama katika Jumuiya hiyo.

Somalia imepata uanachama huo baada ya kuwasilisha hati yake ya kuidhinishwa kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo katika Makao Makuu ya Jumuiya yaliyopo Arusha, Tanzania.

Itakumbukwa kuwa November 2023 mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa EAC uliofanyika Arusha uliridhia Nchi ya Somalia kujiunga na EAC ambapo kwa hatua hii sasa inakuwa Mwanachama wa nane wa Jumuiya hiyo baada ya Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Sudan Kusini, Tanzania, Rwanda na Uganda.

Hatua hii inatajwa kuwa itaimarisha ukuaji wa uchumi wa Somalia ambao bado unaendelea kuimarika kutokana na miongo mitatu ya vita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live