Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Kenya

58be7a59874f1ab4d5e1932037e9e992.png Somalia yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Kenya

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Serikali ya Somalia imewaondoa maofisa wote wa ubalozi nchini Kenya, sambamba na kuvunja uhusiano wa kidiplomasia kutokana na kile taifa hilo walichokiita kuingiliwa uhuru wao

Waziri wa Habari wa Somalia, Osman Abukar Dubbe aliliambia shirika la habari ‘VOA’ kuwa uamuzi huo umechukuliwa kujibu kile alichokiita ukiukaji wa kisiasa wa hivi dhidi ya Kenya.

"Kwa kutimiza wajibu wake wa kikatiba kulinda umoja, enzi kuu na utulivu wa nchi hiyo, imeamua kukata uhusiano wa kidiplomasia na Serikali ya Kenya," alisema Osman Dubbe.

Uhusiano kati ya nchi hizo mbili umedhoofika tangu Novemba 29, wakati Somalia ilipomkumbusha balozi wake Nairobi na kumuamuru balozi wa Kenya kuondoka Mogadishu kwa mashauriano na serikali yake.a

Chanzo: habarileo.co.tz