Somalia. Serikali ya Somalia imetangaza hali ya dharura kutokana na kuenea kwa kundi kubwa la nzige.
Kuenea kwa makundi hayo ya nzige kunahofiwa huenda kusaababisha uhaba wa chakula katika eneo la Afrika mashariki.
Taarifa ya wizara ya kilimo ilisema wadudu hao wameshambulia mazao ya chakula na kufanya hali ya usalama wa chakula nchini Somali kuwa hatarini.
“Kuna hofu kubwa hali hii inaweza ikashindwa kudhibitiwa kabla ya muda wa mavuno mwezi Aprili,” ilisema taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Somalia ambayo imekuwa katika changamoto za hali ya kiusalama kwa muda mrefu haiwezi kutumia dawa ya kunyunyizia kwa kutumia ndege ili kuuwa wadudu hao.
Kwa upande wake Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Chakula na Kilimo (FAO), lilisema uvamizi huo wa nzige katika nchi za Somalia na Ethiopia haujawahi kutokea katika miaka 25 iliyopita.
Pia Soma
- Mbatia, Musukuma wataka Mtume Mwamposa kujadiliwa bungeni
- Katiba ya Tanzania yatajwa kikwazo uraia pacha
- Wagonjwa wa corona wafikia 10 Ujerumani
Kwa mujibu wa FAO, idadi ya nzige hao huenda ikaongezeka mara 500 zaidi ifikapo Juni, mwaka huu.
Mbali na nzige hao kuongezeka maeneo ya Afrika Mashariki pia wamejitokza katika nchi za India, Iran na Pakistan.