Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na Kenya

Ed419b6bbfe83ad633efbc05e6a1aeaf Somalia yasitisha uhusiano wa kidiplomasia na Kenya

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SERIKALI ya Somalia imesitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na nchi jirani ya Kenya.

Nchi hiyo imewaita nyumbani wanadiplomasia wake wote kutoka Nairobi na kuwapatia wanadiplomasia wa Kenya muda wa siku saba kuondoka nchini humo.

Tangazo la hatua hiyo limetolewa na Waziri wa Habari, Osman Abukar Dubbe katika chombo cha habari kinachomilikiwa na serikali na kunukuliwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

"Serikali ya Somalia, kulingana uhuru wake unaotokana na sheria za kimataifa, inatekeleza wajibu kwa mujibu wa katiba ili kulinda utaifa, umoja na ustawi wa nchi. Serikali imeamua kusitisha uhusiano wake wa kidiplomasia na serikali ya Kenya," imesema taarifa ya Waziri.

Hatua hiyo inakuja baada ya Somalia kuwasilisha barua ya malalamiko dhidi ya Kenya kwa Waziri Mkuu wa Sudan, Abdalla Hamdok, ambaye pia ni mwenyekiti wa viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Afrika Mashariki na Pembe ya Afrika (IGAD).

Hivi karibuni Somalia iliituhumu Kenya kwa kuingilia masuala yao ndani nchi hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz