Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Somalia yasherehekea kusamehewa deni la dola bilioni 4.5

Somalia Yasherehekea Kusamehewa Deni La Dola Bilioni 4.5 Somalia yasherehekea kusamehewa deni la dola bilioni 4.5

Thu, 14 Dec 2023 Chanzo: Bbc

Serikali ya Somalia siku ya Jumatano ilifanya sherehe katika mji mkuu, Mogadishu, baada ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia kutangaza msamaha wa deni wa dola bilioni 4.5 kwa nchi hiyo.

Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre anasema kwamba afueni hiyo ni "sawa na kumuondolea kila Msomali deni la zaidi ya dola 300".

"Huu ni ushahidi kwamba nchi yetu na watu wetu wana uwezo wa kifedha, na kuvutia wawekezaji kutoka nje, na hatuko tena kwenye minyororo ya madeni," anaongeza.

Mashirika hayo yalisamehe deni la Somalia chini ya mpango wa Nchi Maskini Wenye Madeni Mengi (HIPC), ambao uliundwa mwaka 1996 kusaidia nchi maskini zinazokabiliwa na mzigo wa madeni usioweza kurekebishwa.

Msamaha wa deni wa $4.5bn pia unajumuisha msamaha wa wadai wengine wa kimataifa, wa nchi mbili na wa kibiashara.

"Deni la nje la Somalia limeshuka kutoka asilimia 64 ya Pato la Taifa mwaka 2018 hadi chini ya asilimia 6 ya Pato la Taifa kufikia mwisho wa 2023," taasisi hizo zilisema katika taarifa yake ya pamoja.

Waziri Mkuu Barre anasema afueni hiyo ni kubwa kwani itairuhusu Somalia kuwekeza katika mipango ya maendeleo, kufufua uchumi na kukopa pesa kutoka kwa taasisi za kimataifa zinazotoa mikopo.

Chanzo: Bbc